Simba SC yataja viingilio dhidi ya Raja Casablanca

NA DIRAMAKINI

UONGOZI wa Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam umetaja viingilio katika mchezo ujao dhidi ya Raja Casablanca.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kiingilio cha chini ya mchezo wao wa pili wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Februari 18, 2023 kitakuwa shilingi 5000.

"Viingilio vimetangazwa mapema ili kuwapa nafasi mashabiki kununua mapema sababu tunahitaji mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanjani kuipa sapoti timu,"imefafanua sehemu ya taarifa hiyo.

Viingilio ni kama ifuatavyo:

Mzunguko Sh. 5000
VIP B & C Sh. 20000
VIP A Sh. 30,000
Platinum Sh. 100,000
Platinum Plus Sh. 150,000

Vitu ambavyo atavipata atayenunua tiketi za Platinum ni;

1. Escort kutoka Hoteli ya Hyatt Regency mpaka uwanjani.

2. Kifurushi maalum kutoka Simba.

3. Chakula na Vinywaji ukiwa uwanjani.

Ili kupata tiketi za Platnum na Platnum Plus wapigie kwa namba hii +255742771311.Tayari tiketi zimeanza kuuzwa kwa njia ya mtandao muda mfupi ujao tutatangaza vituo ambavyo zitapatikana.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news