Simba SC yawaacha Mkude,Mwanuke,Mussa na Okrah Dar

NA DIRAMAKINI

KIKOSI cha Simba kimewasili salama nchini Uganda tayari kwa mchezo wa tatu wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Vipers utakaopigwa Jumamosi hii.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na klabu hiyo,leo kikosi kitafanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa St. Mary’s ambapo mchezo wao huo.

Aidha, taarifa hiyo imeeleza kuwa, hali ya wachezaji ni nzuri na morali ipo juu na kila mmoja yupo tayari kuhakikisha anapambana kuipigania timu kupata ushindi dhidi ya Vipers.

Mchezo huo dhidi ya Vipers utapigwa Jumamosi katika Uwanja wa St. Mary’s wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 15,000 kuanzia saa moja usiku.

Picha na Simba SC.

Kikosi ambacho kipo Uganda kina jumla ya wachezaji 24, benchi la ufundi pamoja na baadhi ya viongozi.

Miongoni mwao ni makipa Aishi Manula,Beno Kakolanya,Ally Salim huku mabeki wakiwa ni Shomari Kapombe,Israel Mwenda,Mohamed Hussein,Gadiel Michael,Kennedy Juma,Mohamed Ouattara,Joash Onyango, Henock Inonga na Erasto Nyoni

Kwa upande wa viungo ni Sadio Kanoute,Mzamiru Yassin,Clatous Chama,Ismael Sawadogo,Saido Ntibazonkiza, Kibu Dennis,Pape Osmane Sakho na Peter Banda.

Aidha, washambuliaji ni John Bocco, Jean Baleke,Moses Phiri na Habibu Kyombo huku wachezaji ambao hawakusafiri ni Jonas Mkude, Jimmyson Mwanuke, Mohamed Mussa, Augustine Okrah.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news