UJAMAA HAUTAKUFA

NA ADELADIUS MAKWEGA

MATINI hapo chini ni mashairi na kiitikio cha wimbo Ujamaa hautakufa, wimbo huo ulipigwa na Kurugenzi Jazz Band ambayo ilikuwa inamilikiwa tuseme kwa sasa Halmashauri ya Jiji la Arusha.

Ukisoma mashairi na ukisikiliza vyombo vilivyopigwa utatambua namna siasa ilivyofanyika kwa umakini, siasa na hamasa, na siasa ya kweli kwa wananchi kutoka mashinani hadi taifa.

Kwa wale wanaopenda muziki rhythm gitaa lilipigwa na mchungaji Joseph Tito ambaye sasa hivi yupo huko Kenya akichunga kondoo kama Mchungaji wa kanisa. 
 
Joseph Tito ni msukuma aliyekulia Tanga katika mashamba ya mkonge. Aliweza kupiga gitaa hilo vizuri katika bendi na nyimbo mbalimbali. 
 
Mathalani wimbo wa Wivu(Kurugenzi Jazz) Ujamaa hautakufa (Kurugenzi Jazz), Twende Vijijini (Kurugenzi Jazz) na Elimu ni Msingi (Kurugenzi Jazz).

Ukiyasoma maishairi hayo vizuri ama ukausikiliza wimbo huo tuni yake utabaini kuwa Watanzania walikuwa Wazalendo wa kweli , tena siyo uzalendo tu, bali uzalendo wa hali ya juu.

Pili, Watanzania hao walikuwa na umoja wa kweli (Real), wengine wakisema kuwa sasa hivi kila mmoja na luwake huku kukiwa na kutamalaki kwa ubinafsi.

Tatu, wengine wanadiriki kusema kuwa sasa kuna kizazi cha nyoka kinapita kinashindwa kuelimisha na kurithisha uzalendo huo kwa watoto wetu. Mathalani hivi sasa hata hiyo bendera ya taifa ikipandishwa na kushuswa hakuna anayesimama au anayeshituka.
 
Hayati Kingunge Ngombale Mwiru alikuwa miongoni mwa Watanzania wanaoenzi sana Ujamaa
……………………………………………………………………………………………………… Matumaini ya wapinga siasa ya Ujamaa, Njama tumia za hali ya juu kupinga Ujamaa

Ujamaa ni mzuri wenye kuleta usawa,Ujamaa hautakufa Tanzania twaulinda

Tutaendelea hatutarudi nyuma,Tulikwishajua matatizo tutashinda

Mawazo sahau Ujamaa hautakufa, Ujamaa oo yoo oohhhhh

Fungeni vibwebwe tujenge Ujamaa, Ujamaa mamama ohhh

Mawazo sahau Ujamaa hautakufa,Ujamaa aaaa hautakufaa ooooh

Fungeni vibwebwe tujenge Ujamaa, Matumaini ya wapinga siasa ya ujamaa

Njama mbinu za hali ya juu kuangusha Ujamaa, Ujamaa ni mzuri wenye kuleta usawa

Ujamaa hautakufa Tanzania twaulinda, Tutaendelea hatutarudi nyumaaaa

Tulikwishajua matatizo tutashindwa , Mawazo sahau Ujamaa hautakufa

Fungeni vibwebwe tujenge Ujamaa, Ujamaa mamaa aahhhh

Mawazo sahau Ujama hautakufa, Ujamaa mama ohhh

Fungeni vibwebwe tujenge Ujamaa.

(Ujamaa hautakufa, Tanzania tutaulinda)

Matumaini yetu wapinga siasa ya Ujamaa, Watumia mbinu za hali ya juu kuangusha ujamaa

Ujamaa ni mzuri wenye kuleta usawa, Ujamaa hautakufa Tanzania twaulinda

Tutaendelea hatutarudi nyuma Tulikwishajua matatizo tutashinda

Mawazo sahau Ujamaa hautakufa, Fungeni vibwebwe tujenge ujamaa

Mawazo sahau Ujamaa hautakufa, Fungeni vibwebwe tujenge ujamaa.
……………………………………………………………………………………………………

“Kaka hayo mambo ya jeshini siyo huku kitaa.” Utasikia wazalendo wa sasa wakijinasibu.

Naweka kalamu yangu chini kwa kusema kuwa tutaendelea kuwakumbuka wanasiasa wa kweli, wawazi kama aliyewahi kuwa katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa TANU marehemu Kingunge Ngombale Mwiru.

makwadeladius@gmail.com
0717649257.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news