NA MWANDISHI WETU
MKUU wa Mkoa wa Tabora, Balozi Dkt.Batilda Salha Burian ameshuhudia zoezi la utiaji saini mkataba wa ujenzi wa mabwawa ya kutibu majitaka unaosimamiwa na TUWASA chini ya Mkandarasi M/S Peritus Exim Private Limited. Zoezi hilo pia limeshuhudiwa na kamati ya ulinzi (M) Tabora na Viongozi wa CCM (M).
Katika hotuba yake, Dkt. Batilda alianza kwa kumshukuru Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha ambazo zinasimamia miradi ya maendeleo kwa mkoa wa Tabora. Na pia alitoa shukrani kwa wizara ya maji na viongozi wa CCM kwa kuisimamia vema Ilani ya CCM ya mwaka 2020.
Aidha, Dkt.Batilda amewataka TUWASA kuweka mifumo bora ya maji kwani tayari serikali imeshatoa fedha Bilioni 640, kutoa maji ziwa Victoria hadi Tabora. Na hivyo kuna kila haja ya kuweka sawa mifumo ya uondoshaji wa majitaka.
Ametoa wito kwa wadau mbalimbali kutoa ushirikiano kwa TUWASA ili kutoa huduma bora kwa wananchi wa Tabora. Lakini pia amewataka TUWASA kusimamia kikamilifu mkandarasi ili mradi huo ukamilike kwa wakati na wenye ubora unaotakiwa.
Amewataka wanatabora kulipa Ankara zao kwa wakati, kulinda miundombinu ya maji ili kuiwezesha TUWASA kutoa huduma bora kwa wananchi wa Tabora.
Naye Mwenyekiti Bodi ya TUWASA, Dick Mlimuka, amemuhakikishia Dkt.Batilda kuwa, kwa kushirikiana na mkandarasi, watasimamia mradi huo na kukamilika kwa wakati uliopangwa.
Na kwamba ujenzi huo utagharimu Billioni moja, million mia sita ishirini na nane, Mia nane thelathini elfu, mia mbili themanini na tisa na senti sabini na sita( 1,628,830,289.76) na utachukua muda wa miezi 12 kukamilika, na kukamilika kwa mradi huo kutaboresha utunzaji wa mazingira.