UNAWEZA KUJARIBIWA

NA ADELADIUS MAKWEGA

WAKRISTO wametakiwa kutambua kuwa katika maisha yao wanaweza kujaribiwa kama alivyofanyiwa Bwana Yesu, kubwa ni kujikabidhi kwa Mungu na majaribu hayo yatashindwa.

Hayo yamesemwa katika misa ya Jumapili ya kwanza baada ya Jumatano ya majivu Februari 26, 2023 iliyofanyika katika Kanisa la Bikira Maria Imakulata, Parokia ya Chamwino Ikulu, Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma na Padri Paul Mapalala Paroko wa Parokia hiyo.
“Katika Kwaresma hii kila mmoja atambue kuwa yapo majaribu yanayataka kumuangusha, kumtengua au yanayojaribu kumpeleka tofauti na misimamo ya dini na misimamo ya mafundisho ya Kristo, daima ujikabidhi kwa Mungu, daima ujikabidhi kwa Kristo. Katika ulimwengu wa sasa majaribu ni mengi, tunatakiwa kufuata mfano wa Kristo daima ambavyo yeye alijikadhi kwa Mungu Baba na yeye ndiye aliyemtuma kuja kuukomboa ulimwengu.”

Misa hiyo ya dominika pia iliambata na maombi kadhaa na mojawapo ni hili, “Eee Bwana Yesu, ulishawishiwa kuchagua njia ya siasa ili kutukomboa, utufundishe kutambua kwamba Ufalme wa Mungu siyo ufalme wa kupigania mamlaka na madaraka, bali kutimiza amri zako.”
Hali ya mahindi yanayonyauka kutokana na jua kali.

Mpaka misa hiyo ya kwanza inamalizika, hali ya hewa ya eneo la Chamwino Ikulu kwa juma zima bado jua kali limetamalaki, huku mahindi ambayo hayabeba chochote yanakauka. Baadhi ya wakulima wakifanya palizi za mazao yao alfajiri kwani wanaogopa wakifanya palizi wakati jua linawaka kunaweza kusababisha mizizi ya mazao hayo kukaushwa na jua na mmea kufa.
Hali ya mahindi ya mbegu ya muda mfupi yanayohitaji mvua moja.
.
Mwandishi wa ripoti hii amebaini kuwa, japokuwa hali iko hivyo, lakini wakulima hao bado wamejawa na matumaini kwa mvua kunyesha hapo mbele, nafuu inaonekana kwa wakulima waliopanda mbegu za muda mfupi dalili zinaonesha wanahitaji mvua moja mahindi hayo yaweze kubeba vizuri.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news