Waziri Dkt.Biteko ateta na wawekezaji kutoka Sweden

NA MWANDISHI WETU

TIMU ya wawekezaji kutoka nchini Sweden ikiongozwa na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mheshimiwa Charilotta Ozaki Makiasi na Mkurugenzi Mkuu wa Scania Lors Eklund wamekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko jijini Dodoma.
Akizungumzia nia ya timu hiyo kuweza katika sekta ya Madini nchini, Balozi Charilotta amesema timu hiyo ipo tayari kuwekeza katika nyanja ya usafirishaji nchini hususan katika sekta ya Madini.
Akieleza kuhusu mahusiano mazuri ya kiuchumi na kidiplomasi yaliyopo baina ya Tanzania na Sweden Balozi Charilotta amesema kuwa kwa kipindi cha miaka 50 Sweden imekuwa na mahusiano mazuri na imekuwa mdau wa maendeleo nchini Tanzania kwa kipindi chote.
Kwa upande wake, Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko amewashauri wawekezaji hao kushiriki mkutano wa Jukwaa la Ushirikishwaji wa Watanzania katika Uchumi wa madini nchini kwa lengo la kujifunza juu ya Sheria , Kanuni, Taratibu za uwekezaji katika sekta ya Madini.
Mapema baada ya mkutano huo Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa amekutana na baadhi ya wajumbe wa kikundi cha Umoja group cha mkoani Geita pamoja na wawakilishi kutoka kampuni ya uchimbaji madini ya Geita Gold Mine Limited (GGML) kwa lengo la kutatua migogoro iliyokuwapo baina ya GGML na wananchi hao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news