Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishuhudia utiaji saini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji kwa vijiji 34 vya wilaya ya Ruagwa na vijiji 21 vya wilaya ya Nachingwea kwa kutumia chanzo cha maji cha Nyangao, kwenye ukumbi wa VETA Nandagala wilayani Ruangwa, Februari 18, 2023. Pichani, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini, Mhandisi Clement Kivegelo (kushoto) na Lawrence Nkya kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya STC Construction Limited wakitia saini mkataba huo. Waliosimama ni Gloria Chegeni , Mkuu wa Kitengo cha Sheria RUWASA na kulia ni Mubarak Juma ambaye ni Mkurugenzi wa Manunuzi wa Kampuni hiyo. Kulia kwa Waziri Mkuu, ni Naibu Waziri wa Maji, Maryprisca Mahundi na kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kushuhudia utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa Miradi wa Maji kwa vijiji 34 vya wilaya ya Ruangwa na vijiji 21 vya wilaya ya Nachingwea kwa kutumia chanzo cha maji cha mto Nyangao. Tukio hilo lilifanyika kwenye ukumbi wa VETA Nandagala wilayani Ruangwa, Februari 18, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).Baadhi ya mwananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipozungumza baada ya kushuhudia utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa mradi wa Maji kwa vijiji 34 vya wilaya ya Ruangwa na vijiji 21 vya wilaya ya Nachingwea kwa kutumia chanzo cha maji cha mto Nyangao. Tukio hilo lilifanyika kwenye ukumbi wa VETA Nandagala wilayani Ruangwa, Februari 18, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).