NA MWANDISHI WETU
WIZARA ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imefanya kikao kazi cha kwanza cha aina yake kupata kufanyika kwa kuwakutanisha maafisa habari wa Wizara na vitengo vilivyo chini yake na kuweka mikakati thabiti ya kuhakikisha taarifa za Wizara na taasisi zake zinatangazwa kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Anthony Ishengoma akiwasilisha maelekezo kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia na Salamu za Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Allan Kijazi kwa Maafisa habari wa Vitengo vya Habari na Mawasiliano vilivyo chini ya Wizara ya Ardhi katika Hoteli ya Edema Mjini Morogoro leo waliokutana kwa ajili ya kubadilishana uzoefu, kujadiliana na kuangalia namna bora ya kutangaza kazi za Wizara na Taasisi.
Kikao kazi hicho cha siku mbili cha Vitengo vya Habari na Mawasiliano vilivyo chini ya Wizara ya Ardhi kwa ajili ya kubadilishana uzoefu, kujadiliana na kuangalia namna bora ya kutangaza kazi za Wizara na Taasisi.
Meneja Habari na Uhusiano wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Muungano Kasibi Saguya akitoa maada kuhusu Uhusiano na Vyombo vya Habari kwa Maafisa habari wa Vitengo vya Habari na Mawasiliano vilivyo chini ya Wizara ya Ardhi katika Hoteli ya Edema Mjini Morogoro leo waliokutana kwa ajili ya kubadilishana uzoefu, kujadiliana na kuangalia namna bora ya kutangaza kazi za Wizara na Taasisi.
Kikao kazi hicho kinafanyika katika Hoteli ya Edema Mjini Morogoro, na kuhudhuriwa na wakuu wa vitengo vya Habari na Mawasiliano/Uhusiano na ambao wanahusika na utoaji wa taarifa kwa umma kupitia vyombo vya habari, uhuishaji katika mitandao ikiwamo tovuti, Instagram, Youtube, Twitter na Facebook.
Mwezeshaji Dereck Murusuri akitoa maada Kutangaza kazi njema za Serikali kwa kupitia Mawasiliano yenye ushawishi kwa Maafisa habari wa Vitengo vya Habari na Mawasiliano vilivyo chini ya Wizara ya Ardhi katika Hoteli ya Edema Mjini Morogoro leo waliokutana kwa ajili ya kubadilishana uzoefu, kujadiliana na kuangalia namna bora ya kutangaza kazi za Wizara na Taasisi.
Masuala mengine yanayojadiliwa katika kikao kazi hicho ni pamoja na kujadiliana namna bora ya utekelezaji wa Maelekezo ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
Pia kujifunza namna sahihi za uwekaji na uwasilishaji taarifa kwenye tovuti pamoja na mitandao ya kijamii kama vile, Instagram, Youtube, Twitter na Facebook.
Kupitia kwa pamoja Rasimu ya Mkakati wa Mawasiliano wa Wizara na taasisi zilizo chini ya Wizara kuwasilisha mpango kazi wa shughuli za mawasiliano kwa umma.
Washiriki wa Kikao Kazi hicho ni Mafisa wanaohusika na mawasiliano na uwekaji taarifa kwenye tovuti na mitandao ya kijamii ya Taasisi zilizo chini ya Wizara kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Kitengo cha Mawasiliano Wizarani (GCU), Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi (NLUPC), Bodi ya Usajili wa Wataalamu wa Mipango Miji (TPRB), Bodi ya Uthamini wa Wathamini (VRB), Chuo cha Ardhi Morogoro (ARIMO) na Chuo cha Ardhi Tabora (ARITA).