Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia yaanzisha Kituo cha Huduma kwa Mteja

NA MWANDISHI WETU

WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeanzisha Kituo cha Huduma kwa Mteja kitakachowawezesha Watanzania kutoa taarifa na kufanyiwa kazi kwa wakati.
Akitangaza namba za Kituo hicho jijini Dodoma Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Francis Michael amesema namba hizo zitakuwa zikipokea maulizo, malalamiko na taarifa zozote za ukiukwaji wa taratibu na miongozo ya utoaji elimu ikiwemo ukatili kwa wanafunzi shuleni na vyuoni.

"Mambo yote ya ukatili na uvunjifu wa maadili kwa wanafunzi shuleni na vyuoni yatapokelewa kupitia namba hizo na niwahakikishie mtu yeyote atakayetoa taarifa atalindwa na taarifa zake zitakuwa za siri," amesema Katibu Mkuu Michael.

Katibu Mkuu Michael amesema kituo hicho kitakuwa wazi kuanzia saa 2:00 asubuhi mpaka 10:00 jioni na namba za kutoa taarifa ni 026 2160270 na 0737 962965.

Kiongozi huyo amesema kuanzishwa kwa kituo hicho ni katika kuendelea kuboresha utoaji wa huduma za elimu kwa Watanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news