Yasiyowezekana kwa mwanadamu yupo Mungu wa Mbinguni

NA MWANDISHI WETU

WAADVENTISTA Wasabato wameambiwa wasikae kwenye viti vya malalamiko wainuke, Yesu amewakomboa, yasiyowezekana kwa mwanadamu yupo Mungu wa mbinguni anaweza kuyafanya endapo watakuwa tu na Imani ya Kuponywa.

Hayo yamesemwa na Mchungaji Ndola wa Kanisa la Waadventista Wasabato katika ibada iliyofanyika ndani ya ukumbi wa Chimwaga jijini Dodoma Jumamosi 18, Februari 2023. Mchungaji aliyasema hayo wakati akihudumu ambapo Mzee wa kanisa Elisante Enea alisoma fungu kuu kwa unyenyekevu mkubwa, Matendo 14: 8-10 na wimbo 108 katika kitabu cha Nyimbo za Kristo uliimbwa kwa utulivu kusindikiza fungu hilo.

Ibada hiyo iliambatana na ombi maalumu kutoka kwa mchungaji Bunga Edward Dettu ambapo Waadventista Wasabato hao wakiwa ni wanafunzi wa Shahada ya kwanza na Shahada ya umahiri waliwekwa mikononi mwa Bwana kwa ajili ya Mitihani ya Chuo Kikuu inayoanza mapema Jumatatu tarehe 20 Februari 2023.

Pia, katika kuwezeha huduma kwa watu wenye mahitaji maalumu zaidi ya Waadventista Wasabato 50 walitambuliwa na kupongezwa kwa kuhitimu mafunzo ya awali ya lugha ya alama.

Naye Mchungaji Ndola aliwasisitza wahitimu hao watumia elimu yao kuwafikia watu wenye mahitaji maalumu maana dini safi nikuwasaidia watu katika dhiki zao, Yakobo 1:27.

Wakati ibada inaendelea ndani ya ukumbi huo ghafla umeme ulikatika, likatawala giza nene mithili ya kupatwa kwa jua kikamilifu takribani kama sekunde 78 ndipo umeme uliwaka nuru ikarejea na ibada ikaendelea.

Katika ibada hiyo, kwaya za makanisa zilihudumu kwa ubora wa hali ya juu ambapo ukurasa wa ibada ulifungwa kwa wimbo wa Kwaya ya Canan saa saba na dakika kadhaa mchana.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news