NA DIRAMAKINI
CHAMA cha ACT Wazalendo kimesema kitaendelea na mikutano ya hadhara na kutangaza ya Brand Promise yake katika awamu ya pili ambayo itaanza Mei 4 hadi 13, mwaka huu katika mikoa tisa ya Tanzania Bara.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kutoa mrejesho wa majumuisho ya mikutano mara baada ya kuhitimisha awamu ya kwanza, Katibu Mkuu wa chama hicho, Ado Shaibu amesema, ratiba ya mikutano ya hadhara ya awamu ya pili itaanzia mkoani Ruvuma na kumalizia mkoani Mwanza.
Anesema, mikoa itakayofanyika mikutano hiyo kuwa ni Ruvuma, Njombe, Rukwa, Katavi, Mkoa wa Kichama Kahama, Geita, Shinyanga, Simiyu na Mwanza.
Awali akitoa mawasilisho ya awamu ya kwanza ya Mikutano ya Hadhara waliyofanya maeneo mbalimbali nchini Waziri Mkuu Kivuli wa chama hicho , Dorothy Semu amesema huduma duni za afya ni changamoto kwa wananchi.
Aidha, amesema Chama cha ACT Wazalendo kimeishauri Serekali ilete maboresho ya sheria kuhusu mifuko ya hifadhi ya jamii PSSF na NSSF ili wananchi watumie kupata huduma za afya kwa kuchangia elfu ishirini kwa mwezi na serikali ichangie elfu kumi.