NA MWANDISHI WETU
BALOZI wa Tanzania nchini Malta mwenye makazi yake Roma nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo amewasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Malta, Mheshimiwa Dkt. George Vella katika Ikulu ya Malta.


Uhusiano wa kidiplomasia baina ya Tanzania na Malta ulianza mwaka 2015 na tangu wakati huo, juhudi za kukuza uhusiano huo zimekuwa zikifanyika kupitia sekta za elimu, utalii na usafiri wa anga; na kupitia katika majukwaa ya kimataifa ya Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Madola ambazo nchi zote mbili ni wanachama.