Bondia Karimu Mandonga (Mtu kazi) apewa Ubalozi Kampuni ya Nyumba Fasta

NA DIRAMAKINI

BONDIA wa ngumi maarufu Tanzania, Karimu Mandonga (Mtu kazi) amepata dili ya ubalozi kutoka Kampuni ya Nyumba Fasta.
Ubalozi wake umetangazwa kupitia tukio lilofanyika katika ofisi za Nyumba Fasta zilizopo Kijitonyama Victoria jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Kampuni ya Nyumba Fasta imempa ubalozi kwa kuwa ana vigezo vyote vya kufanya kazi nao huku wakitambulisha mfumo mpya wa kidigitali.

Waandishi wa habari wameweza kumuuliza Karim Mandonga siri ya mafanikio yake ya kupata dili za ubalozi mfululizo ikiwemo hili dili kubwa la ubalozi wa kampuni ya Nyumba Fasta

Mandonga akijibu swali hilo amesema "Wakati wa Mungu ni wakati sahihi, Mwenyenzimungu Ana uwezo wake, hivyo kupewa ubalozi wa Nyumba Fasta ni uwezo wa Mungu"

Pia Karimu Mandonga ametambulisha ngumi yake mpya inaitwa Mlungambunga ambayo imetokana na Jangwa la Sahara inayompoteza mtu hewani.

Naye Meneja Masoko kampuni ya Nyumba Fasta, Robbison Marley amesema mfumo wa nyumba fasta ni mfumo wezeshi ambao utawasaidia watu wa chini na wa kawaida ambao wanaotaka nyumba nzuri na kiurahisi, mfumo huu hauna malipo ya dalali, kwani kupitia simu yako ya mkononi utakuwezesha kupata nyumba nzuri kwa muda mwafaka.

"Nyumba Fasta ni mfumo wa kidijitali unaokuwezesha kupata nyumba za kupanga bila malipo ya kodi ya mwezi mmoja na kupata mawasiliano ya mwenye nyumba moja kwa moja kwa gharama ndogo kuanzia shilingi elfu moja vilevile nyumba fasta inakuwezesha kununua au kuuza nyumba au ardhi zilizohakikiwa ili kujiepusha na migogoro.

"Nyumba Fasta imetengenezwa na vijana wa kitanzania na inapatikana mtandaoni Tanzania nzima kupitia tovuti kwa kutumia simu janja (smartphone) mwenye nyumba anaweza kusajili nyumba yake na mpangaji anaweza kutafuta nyumba ya kupanga kokote pale Tanzania,"Alieleza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news