NA FRESHA KINASA
MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara, Prof. Sospeter Muhongo ametoa wito kwa wadau mbalimbali kujitokeza kuwasaidia ikiwemo kuwachangia wavuvi wa jimbo hilo walioharibiwa mitumbwi na makokoro yao kufuatia dhoruba ya mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali.
Juzi, Machi 20, 2023 upepo wenye kasi kubwa na mvua kubwa vilisababisha kuwepo kwa dhoruba kubwa ndani ya Ziwa Victoria.Mialo ya Musoma Vijijini ilikumbwa na dhoruba hiyo na uharibifu mkubwa umefanyika.
"Tunaomba tushirikiane kuwachangia wavuvi wetu walioathirika na janga hili. Tathimini ya uharibifu huu inaonesha kuwa,mitumbwi ya Mwalo wa Kijiji cha Busekera iliyoharibika ni 137, inayotengenezeka ni 108,isiyotengenezeka ni 29.
"Aidha, makokoro ya dagaa yaliyoharibika ni 29, mitumbwi ya Mwalo wa
Kijiji cha Buira iliyoharibika ni 39, inayotengenezeka ni
29,isiyotengenezeka ni 10 na makokoro ya dagaa yaliyoharibiwa ni
15,"amefafanua Mbunge Prof.Muhongo kupitia taarifa iliyotolewa leo Machi
22, 2023.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mitumbwi ya Mwalo wa
Kijiji cha Bwai Kumsoma iliyoharibika ni 25, inayotengenezeka ni 21,
isiyotengenezeka ninne huku makokoro ya dagaa yaliyoharibika yakiwa ni
15.
Aidha, kwa upande wa mitumbwi ya Mwalo wa Kijiji cha Kasoma tathimni inaonesha kuwa, iliyoharibika ni 10,inayotengenezeka ni tisa,isiyotengenezeka ni moja huku makokoro ya dagaa yaliyoharibika yakiwa ni matatu.
Wakati huo huo, grahama za matengenezo tathimini inaonesha kama ilivyo mifano ya hapa chini ambayo inakupatia picha unayoweza kuitumia kutoa mchango wako;
(1) Gharama za kutengeneza Mtumbwi
Tsh 1,700,000
Ubao 1 wa 9"x10"
Tsh 12,000
(2) Gharama za kutengeneza Kokoro la Dagaa
Tsh 1,400,000
UWASILISHAJI WA MCHANGO WAKO
Tafadhali mpelekee:
DC Wilaya ya Musoma
Simu: 0756 088 624
Michango ya awali:
Kwa mujibu wa taarifa hiyo,wataanza kuwasilisha michango ya awali kwa wavuvi waathirika siku ya Alhamisi ya Machi 30,2023.
Baadhi ya picha zinaonesha sehemu ndogo ya uharibifu uliofanyika kwenye Mwalo wa Kijiji cha Busekera, Kata ya Bukumi, Musoma Vijijini.