NA MWANDISHI WETU
KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. Jim Yonazi akutana na kufanya mazungumzo na Menejimenti ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) mapema Machi 10, 2023 katika ukumbi wa mikutano Ofisi hiyo Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. Jim Yonazi akizungumza na menejimenti ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania alipokutana nao mapema Machi 10, 2023 jijini Dodoma.
Lengo la kikao hicho ni kumpitisha Katibu Mkuu huyo kuhusu Muundo na utendaji wa Tume ikiwa ni sehemu ya ratiba yake kukutana na Idara na Taasisi zote zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS Dkt. Leonard Maboko akieleza kuhusu muunda wa Tume wakati wa kikao cha Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi alipokutana na timu ya menejimenti ya Tume Jijini Dodoma Machi 10, 2023.
Dkt. Yonazi alitumia nafasi hiyo kuipongeza Tume kwa kazi nzuri wanazofanya na kuwaeleza ni muhimu kuongeza kasi zaidi katika kuyafikia malengo na kuhakikisha jamii inapata huduma na elimu kadiri iwezekanavyo.
Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa TACAIDS, Yasin Abbas akichangia jambo katika kikao cha Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu alipokutana na menejimenti ya Tume hiyo jijini Dodoma.
“Ninawapongeza TACAIDS kuendelea kusaidia katika mapambano haya na kila jitihada zinazofaywa zina tija katika kuyafikia malengo hivyo, tuendelee kutoa elimu kwa umma kwa kuzingatia kuwa mnayagusa maisha watu,”alisema Dkt. Yonazi.
Mkurugenzi wa Habari na Uraghibishi TACAIDS, Bw. Jumanne Isango akizungumza jambo wakati wa kikao hicho.
Wajumbe wa Menejimenti kutoa Tume ya Kudhibiti UKIMWI nchini (TACAIDS) wakifuatilia wakati wa kikao hicho.(Picha na OWM).
Aliongezea kuwa, Ofisi yake ipo wazi na itaendelea kutoa ushirikiano kwa Tume hiyo kwa kuzingatia umuhimu wa shughuli zinazotekeleza na tume.