Fedha za kigeni zipo za kutosha kuagiza bidhaa na huduma-MPC

NA GODFRE NNKO

KAMATI ya Sera ya Fedha (MPC) imebainisha kuwa, Taifa lina akiba ya kutosha ya fedha za kigeni kwa ajili ya kuagiza bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi kwa miezi isiyopungua minne.

Hayo yamebainishwa leo Machi 14, 2023 na Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Emmanuel Tututba kupitia tamko la MPC ambayo ilikutana leo kwa lengo la kutathmini utekelezaji wa sera ya fedha katika miezi Januari na Februari 2023.

Sambamba na mwenendo wa uchumi, na kufanya maamuzi ya mwelekeo wa utekelezaji wa sera ya fedha kwa miezi miwili ijayo.

"Akiba ya fedha za kigeni ilifikia dola za Marekani bilioni 4.8 mwishoni mwa mwezi Januari 2023, kiwango kinachotosheleza uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi kwa miezi 4.3, ikilinganishwa na lengo la nchi la miezi isiyopungua minne,"imefafanua sehemu ya taarifa hiyo ya MPC iliyotolewa na Gavana Tutuba.

Aidha, kwa mujibu wa MPC katika vipindi vijavyo, urari wa biashara ya bidhaa, huduma na uhamishaji mali nchi za nje, pamoja na idadi ya miezi ya uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi, vinatarajiwa kuimarika kutokana na kuendelea kuimarika kwa mnyororo wa ugavi na matarajio ya kupungua kwa bei za bidhaa katika soko la Dunia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news