Fedha za Mfuko wa Jimbo Musoma Vijijini zaendelea kufanya makubwa

NA FRESHA KINASA 

WAKUU wa shule za sekondari za Musoma Vijijini mkoani Mara na bodi zao za shule wameanza kuchukua vifaa vya ujenzi vilivyonunuliwa kupitia fedha za mfuko wa jimbo. 
Hayo yamebainishwa Machi 25, 2023 kupitia taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara, Prof. Sospeter Muhongo. Ambapo taarifa hiyo imesema vifaa hivyo vimeanza kuchukuliwa Machi 24, 2023. 

Manunuzi yalifanywa na Halmashauri yetu (Musoma DC) kama ifuatavyo:

Jumla ya Fedha: 

Tsh 75,796,000

Saruji Mifuko (50%)

1,613

Mabati (40%)

947

Nondo (10%)

337

"Vifaa hivyo vitatumika kuanza ujenzi na ukamilishaji wa Maabara 3 za Masomo ya Sayansi (Physics, Chemistry & Biology) kwenye Sekondari zilizogawiwa vifaa hivyo (rejea taarifa yetu ya awali kuhusu suala hili kwa kutembelea tovuti ya jimbo letu: www.musomavijijini.or.tz).

"Kuwepo kwa Maabara 3 za Masomo ya Sayansi kwenye Sekondari zetu zote 25 za Kata ni sehemu ya matayarisho ya kuanzisha *HIGH SCHOOLS za Masomo ya Sayansi kwenye baadhi ya Sekondari hizo,"imeeleza taarifa hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dkt. Halfan Haule amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuziwezesha Ofisi za wabunge kuwa na fedha za mfuko wa jimbo kwani zimekuwa zikisaidia katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo kwa wananchi. 

"Namshukuru Rais wetu Dkt.Samia Suluhu Hassan kuziwezesha Ofisi za Wabunge kuwa na hizi fedha za mfuko wa jimbo, kwani zimekuwa zikisaidia sana kwa kushirikiana na nguvu za wananchi pamoja na Serikali kuhakikisha vipaumbele vya jimbo vinatekelezwa kwa ufanisi." Amesema Dkt. Haule.

"Tunawashukuru Wananchi pia kwa juhudi zao wanajenga madarasa, lakini tuna changamoto za maabara za Sayansi. lazima tuwawekee mazingira mazuri wasome kwa ufanisi. Nimpongeze Profesa Muhongo yeye ameenda mbali zaidi pamoja na kutumia fedha za mfuko wa Jimbo amekuwa akishirikisha marafiki zake, anatumia fedha zake mfukoni kwenye ujenzi wa Zahanati, shule, kusaidia maafa na miundombinu mbalimbali." amesema Dkt. Haule na na kuongeza kuwa. 

"Nikuhakikisha Mheshimiwa Mbunge, vifaa hivi tutavisimamia vinapofika maeneo husika vianze kazi. Safari imeanza niseme kwamba baada ya mwezi mmoja tutapita kuvikagua tukikuta unavyo tutahamisha na kuvipeleka maeneo mengine ambako wanavililia na hawakupata fursa hii.nimpongeze sana Mbunge kwa kazi nzuri na bidii anazofanya kwa ajili ya Wananchi,"amesema Dkt. Haule. 

Kwa upande wao baadhi ya walimu wakizungumza katika zoezi hilo la uchukuaji wa vifaa hivyo wamesema kuwa faida za kuwa na Maabara katika shule ni pamoja na kuwezesha wanafunzi kwa kuwaandaa kuwa wadadisi katika utatuzi wa changamoto zilizopo, kuwawezesha wanafunzi kuwa na uelewa na ufaulu mzuri kwenye masomo ya Sayansi pamoja na kuwaandaa kwenda kwenye ushindani wa uchumi wa kimkakati 

Pia, wamesema mfuko wa Jimbo kwa kiasi kikubwa umesaidia katika ujenzi wa vyumba vya madarasa na vyumba vya maabara katika shule mbalimbali za Sekondari jimboni humo Jambo ambalo linachochea Mapinduzi chanya katika sekta ya elimu Musoma Vijijini chini ya usimamizi madhubuti na uwajibikaji wa mbunge wao Prof. Muhongo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news