NA MWANDISHI WETU
MASHINDANO ya Sodo 4 Climate ya Betika yameendelea kushika kasi katika viwanja vya Coco Beach jijini Dar es Salaam, katika mashindano hayo timu ya Friends of Tulia Trust imeondolewa na timu ya Espanyol kwa kipigo cha mabao 2-0 kwa upande wa wanaume na mabao 2-1 kwa upande wa wanawake na hao hao Espanyol.
Kikosi cha timu ya wanaume cha Friends of Tulia Trust ambacho tayari kimeaga mashindano hayo ya Sodo 4 Climate ambayo yameandaliwa na Kampuni ya Michezo ya kubashiri ya Betika.
Afisa Habari wa Betika, Juvenalius Rugambwa amesema, mashindano hayo yenye lengo mahsusi kuikumbusha jamii umuhimu wa kutunza mazingira yanaendelea katika viwanja hivyo vya Coco Beach, Dar es Salaam huku kila siku ya Jumamosi michezo mbalimbali inapigwa kwenye viwanja hivyo.
Kikosi cha timu ya Wanawake cha Friends of Tulia Trust ambacho tayari kimeaga mashindano hayo ya Sodo 4 Climate ambayo yameandaliwa na Kampuni ya Michezo ya kubashiri ya Betika.
“Mashindano haya yanahamasisha kutunza mazingira na tayari tumetoa vifaa, elimu ili kutunza Bahari sanjari na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ambayo yamekuwa ni tatizo kubwa duniani kote,” amesema Rugambwa.
Sodo 4 Climate ni mashindano ambayo yanachezwa kwa mpira maalum wa kufuma. Kaulimbiu ya mashindano hayo ni ‘Shabiki Soka, sio uharibifu wa mazingira,' mashindano yanachezwa kwa mfumo wa mtoano (Knock Out).