NA DIRAMAKINI
SHIRIKA la Hope for Girls and Women in Tanzania (HGWT) linalojishughulisha na mapambano ya ukatili wa kijinsia Mkoa wa Mara chini ya Mkurugenzi wake, Rhobi Samwelly limezindua Programu ya Kuwawezesha Wajane kwa kuwajengea uwezo katika masuala ya kiuchumi, kiroho, kisheria na kuwaunganisha pamoja inayotambulika kwa jina la 'Erasto Widows Empowerment Programme.'

Mkurugenzi wa Shirika la Hope for Girls and Women in Tanzania, Rhobi Samwelly amesema, programu hiyo inalenga kuwajenga wajane kiakili, kiroho na kisaikolojia katika kuhakikisha wanashiriki katika mambo mbalimbali kwa ajili ya maendeleo yao na Jamii kwa ujumla.


