Huu hapa utajiri wa Mheshimiwa Ally Salum Hapi

NA DIRAMAKINI

SEKTA ya Kilimo hapa nchini ni muhimili wa maendeleo ya uchumi. Sekta hii inachangia kiasi cha nusu ya pato la Taifa, robo tatu ya bidhaa zinazouzwa nje ya nchi na chanzo cha chakula pamoja na utoaji wa fursa za ajira zaidi ya asilimia 75 ya Watanzania.
Aidha, kilimo kina uhusiano na sekta zisizo kuwa za kilimo kupitia uhusiano wa usafishaji kwenda kwenye usindikaji wa mazao ya kilimo, matumizi na uuzaji nchi za nje.

Pia sekta hii inatoa malighafi kwa viwanda na soko kwa bidhaa zilizotengenezwa. Tanzania inazalisha takribani asilimia 97 ya mahitaji yake ya chakula. Uzalishaji wa mazao ya chakula unatofautiana mwaka hadi mwaka kutegemea kiasi cha mvua kilichopatikana.

Licha ya maendeleo ya kilimo kuwa chini ya Serikali kwa kipindi kirefu, marekebisho ya uchumi kwa jumla yamekuwa na yanaendelea kuwa na matokeo ya muhimu kwenye sekta ya kilimo. 

Marekebisho ya kiuchumi yamesababisha kufunguka sekta hiyo kwa uwekezaji binafsi katika uzalishaji na usindikaji , uagizaji pembejeo za kutoka nchi za nje na usambazaji na masoko ya kilimo. Serikali imebaki na kazi ya usimamizi na usaidizi wa umma na dhima ya uwezeshaji. 

Mheshimiwa Ally Salum Hapi ni miongoni mwa wadau muhimu katika sekta ya kilimo hapa nchini ambao kupitia kazi zao huko mkoani Iringa, matokeo chanya yameendelea kuonekana na chini ni picha zikionesha sehemu ya majukumu yake ambayo yanamtengenezea kipato kizuri;
Picha zote kwa hisani ya Ally Salum Hapi (Twitter), ukihitaji kujifunza mengi kutoka kwa Mheshimiwa Hapi kuhusu kilimo usisite kumtafuta kupitia mitandao yake ya kijamii, utapata maarifa ya kukuvusha kupitia Sekta ya Kilimo na Ufugaji nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news