NA DIRAMAKINI
VIJANA waliotakiwa kuripoti makao makuu ya Polisi jijini Dodoma wanapaswa kuripoti Shule ya Polisi Moshi mkoani Kilimanjaro kesho Aprili Mosi, 2023.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya mabadiliko ya kuripoti iliyotolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IJP Camillius Wambura kutoka makao makuu ya Jeshi la Polisi.
"Vijana hao watatakiwa kuripoti kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Aprili 1, 2023 saa 12:00 asubuhi na sio makao makuu ya Polisi Dodoma kama ilivyotangazwa hapo awali,"imefafanua sehemu ya taarifa ya IJP.
Pia vijana hao wameelekezwa kutunza tiketi za mabasi kwa ajili ya kurejeshewa nauli zao pindi watakapowasili Shule ya Polisi Moshi.
"Sambamba na hilo, vijana waliofanya usaili makao makuu ya Polisi Zanzibar na katika mikoa ya Tanzania Bara utaratibu utabakia kama ulivyotangazwa awali,"imeongeza sehemu ya taarifa hiyo.