NA MWANDISHI WETU
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imepokea na kujadili muundo wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) nchini.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akizungumza wakati wa semina ya kuwajengea uwezo Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria iliyotolewa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Ukumbi wa Bunge Machi 20, 2023 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama akifafanua jambo wakati wa semina hiyo.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakifuatilia semina iliyotolewa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kuhusu muundo wa Mamlaka hiyo na majukumu yake katika Ukumbi wa Bunge Machi 20, 2023 jijini Dodoma.
Kamishna wa Kinga na Tiba kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Dkt. Peter Mfisi akiwasilisha muundo wa taasisi hiyo na majukumu yake kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria katika Ukumbi wa Bunge Machi 20, 2023 jijini Dodoma.
Kamishna wa Sheria kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Bi.Veronica Matikila akitoa wasilisho kuhusu sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Namba 5 ya mwaka 2015 mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria katika Ukumbi wa Bunge Machi 20, 2023 Jijini Dodoma.(Picha na OWM).
Kikao hicho kilichofanyika Machi 20, 2023 Jijini Dodoma kimeongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama na kuhudhuriwa na wajumbe wa Kamati hiyo pamoja na wadau mbalimbali.