SIMULIZI YA KUTISHA KATIKA MAISHA-6

NA WILLIAM BOMBOM

Ilipoishia ...ule unga ulikusanywa na mtoto THE BOMBOM kisha ukahifadhiwa kwenye chombo fulani. Ikafuata zamu ya mchawi mwingine, alishikwa na kusogezwa eneo husika. Machozi yakawa yanamtiririka mfano wa chemichemi za mto Simiyu. Bibi hakujali hilo aliendelea kumvuta.

Endelea

Mambo hayo yalifanyika mchana kweupe tena nyumbani kwa bibi, hakuna mwanafamilia hata mmoja aliyekumbuka kuingia ndani ya nyumba hiyo. 
Dawa iliyokuwa imemwagwa kuzunguka nyumba hiyo iliwazuia kuingia ndani ya nyumba hiyo. Hatimaye bibi alimfikisha mchawi huyo eneo husika, hakuwa na namna yeyote ya kujinasua toka mikononi mwa bibi. 

Mambo hayo hayakuwa mazuri machoni mwa wale wachawi sita waliokuwa wamebakia. Kabla bibi hajafanya jambo lolote dhidi ya mchawi huyo, mtoto THE BOMBOM alimsogelea mchawi huyo kisha akaunyanyua mkono wake na kuusogeza kichwani mwa mchawi huyo. 

Alipapasa mikono yake huku ikielekea sehemu ya macho ya mchawi huyo, alipofika sehemu ya macho alikamata jicho moja na kuanza kuling'oa. 

Yule mchawi alijaribu kupiga kelele kulingana na maumivu aliyokuwa akiyasikia. Lakini mtoto THE BOMBOM hakujishughulisha na kilio chake, aliendelea kulivuta jicho hilo hatimaye akalinyofoa kabisa. Damu zilitiririka mithili ya kondoo aliyechinjwa.

Jicho lilirukaruka mithili ya mkia wa mjusi uliokatwa. Maumivu yalikuwa makali yasiyo na mfano, aliendelea kupiga kelele lakini hakupata msaada wa aina yeyote. 

Hapa niseme kidogo, ndugu msomaji mara nyingi unapotembea wakati wa usiku huwa unakutana na wachawi. Kwa kuwa hauna jicho la pili ni vigumu kuwaona, siku zote wachawi huzungumza kwa sauti za juu wanapokuwa wanawasiliana. 

Hii ndiyo kanuni na sheria za madawa wanayotumia, endapo utazungumza sauti ya chini ni rahisi kwa mtu yeyote kuisikia sauti hiyo hata kama hauna madawa.

Mara nyingi kanuni za kichawi hutofautiana na kanuni za kawaida za binadamu. Mfano mmojawapo ni huo wa kuongea kwa sauti ya juu, ilihali katika mazingira ya kawaida huwa tunazungumza taratibu. 

Mfano mwingine ni uvaaji, unapotembea wakati wa usiku upende kubadili nguo zako nje ndani. Kuanzia nguo za ndani hadi nje hakikisha unazigeuza, hii inaweza kuwa salama kwako na utanishukuru.

Kwa namna hiyo kelele za yule mchawi aliyekuwa kang'olewa jicho, hazikusaidia kitu chochote katika mazingira hayo. 

Aliliweka vyema jicho hilo mkononi mwake, kisha akalirushia mdomoni mwake na kulitafuna taratibu. Katika umri huo mtoto THE BOMBOM alikuwa alishazoea mambo hayo, pengine kuna mambo mazito zaidi ya hayo alikuwa alishayafanya. 

Alikuwa ni mtoto wa ajabu kuwahi kutokea, muda mwingine alifanya mambo mazito hadi bibi yake akashangaa. 

Wakati hayo yakiendelea ghafla kulisikika kelele za misukule juu ya dari, misukule hao walikuwa wakigombania kushuka chini lakini wakawa wanaogopa. Walibaki wakipiga kelele huku wakichungulia kwa chini. 

"Tata yamaaaaaaaa! Tata yamaaaaaaaa! Tata yamaaaaaaaaaaaaa! Zilikuwa ni sauti za misukule waliokuwa wakizungumza kwa sauti wakiomba nyama. 

Kwa kuwa huwa wamekatwa ulimi hivyo basi baadhi ya maneno hawawezi kuyatamka. Badala ya nataka wao husema tata, vivyo hivyo badala ya nyama wao husema yama. 

Ndugu msomaji kama nilivyoeleza hapo mwanzo, misukule hao walikuwa ndani ya nyumba ya bibi yake mtoto THE BOMBOM. Ni vigumu sana kuwaona misukule kwenye maeneo yao, endapo nyumbani kwenu ni miongoni mwa maeneo ya kutunzia misukule hata ufanyeji huwezi kuwaona. 

Kuna dawa iitwayo ihomoja ambayo hutumiwa kuzima kila kitu nyumbani hapo, kwa hiyo misukule wanaweza kuendelea na mambo yao na ninyi katika familia mkaendelea na mambo yenu pasipo kujua. 

Ni muhusika pekee ndiye huwa na uwezo wa kujua kila jambo linaloendelea katika familia hiyo. 

Zipo sehemu mbalimbali ambazo hutumiwa na wachawi kuhifadhi misukule, sehemu hizo ni pamoja na: miti mikubwa, majengo ya zamani yaliyobaki mapagala, makanisani, misikitini, mashuleni, maorini, mitoni, mabohari, makabirini na kwenye miji ya watu.

Wale misukule walikuwa wamemuona mtoto THE BOMBOM akitafuna jicho la yule mchawi, ndiyo maana wakawa wanapiga kelele wakitaka kula nyama. 

Misukule hao walikuwa wakimuogopa sana bibi maana kuna muda alikuwa akiwaadhibu ikapelekea wao kumuogopa. Ghafla mtoto THE BOMBOM alipeleka mkono wake tena chini ya kitovu cha mchawi. 

Ikumbukwe mchawi huyo alikuwa ni wa kiume, mkono huo ulipitiliza hadi kwenye kenda. 

Alizishika kende hizo na kuanza kuzivuta kwa nguvu, hatimaye alifanikiwa kuzinyofoa huku zakali ikibaki eneo lake. 

Ndugu msomaji usiombe ukakutana na mchawi wa mfano wa mtoto huyu, huwa na roho mbaya zaidi ya shetani. 

Alizining'iniza mikononi mwake zikiwa zimetaakaa damu, alianza kuzitafuna mfano wa msafiri wa garimoshi alaye mishikaki ya Saranda. Bibi alikuwa akifurahia kila jambo lililokuwa likifanywa na mjukuu wake mtoto THE BOMBOM. 

Katika mazingira ya kawaida mtoto huyu alikuwa mpole kuliko kawaida, ni kawaida ya watu wa karba yake kuwa hivyo. 

Hakuna mchawi mkorofi wa waziwazi ndani ya jamii, huwa ni wapole wasiopenda makuu. 

Ni rahisi kumchapa makofi mchawi wakati wa mchana wala asirudishe kitu, majibu yake utayapata baadaye anapokuwa kwenye anga zake. Ni watu wabaya wasio na huruma hata kidogo, ndiyo maana mtoto huyu alikuwa akiyafanya mambo haya pasi na huruma.

Aliendelea kutafuna kende hizo mpaka alipozimaliza, baada ya hapo aliingiza tena mkono eneo la zakali akaishika na kuinyofoa kwa nguvu. 

Wale wachawi sita waliokuwa wamebakia walikuwa wakijutia maamuzi yao. Walimlaumu yule padri mzungu lakini haikusaidia, tayari walikuwa wameshanasa. 

Mbaya zaidi walikuwa wamenasa kwenye mtego mbaya, hawakuwa na namna ya kujinasua mikononi mwa bibi na mtoto THE BOMBOM. 

Kilichokuwa kikitokea mbele yao kiliwatia wasiwasi mkubwa, wakabaki wamejiinamia mithili ya shekhe aliyekamatwa ugoni akidhini na mke wa Imamu.

Mtoto THE BOMBOM aliendelea kuzitafuna zakali pasi na wasiwasi, wale misukule wakabaki wakimkodolea macho mtoto huyo. 

Walitamani sana nyama hiyo lakini hawakuwa na jinsi, wakabaki wakichungulia toka darini huku udenda ukiwatoka. 

Tayari mchawi huyo alikuwa ameshaaga dunia, mateso aliyopitia ilikuwa ni siri yake. Bibi alimgeuza vizuri mchawi huyo kisha akauvuta ulimi wake, aliuvuta! akauvuta! Akauvuta! Hatimaye alifanikiwa kuunyofoa mzima mzima. 

Baada ya hapo waliuchukua mwili wa mchawi huyo kisha wakairushia juu ya dari, wale misukule wakaendelea kumnyofoa kiungo kimoja baada ya kingine huku wakifurahia nyama tamu. Ikafika zamu ya mchawi mwingine, safari hii mtoto THE BOMBOM aliwasogelea ili aweze kichagua zamu ya mmoja wao. Wakati akiwasogelea.

Ndugu msomaji mtoto THE BOMBOM ameshaanza mambo yake, je hili KANISA LA KICHAWI lina uhusiano gani na mtoto huyo? Tafadhali endelea kufuatilia kisa hiki cha kusisimua.

MIDIMU!

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news