Kasulu kukabiliana na tatizo la wanafunzi wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu

NA RESPICE SWETU

IDARA ya Elimu Awali na Msingi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, imedhamiria kupambana na tatizo la kuwepo kwa wanafunzi wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu ili kuwawezesha wanafunzi wanaofanya mitihani katika halmashauri hiyo, kufanya vema kwenye mitihani yao.
Mwalimu Charles Peter wa Shule ya Msingi Nyanchenda akiwafundisha wanafunzi wake kuhesabu.

Hali hiyo imebainika wakati wa zoezi la kufuatilia utendaji kazi wa walimu linaloendelea katika halmashauri hiyo ili kuona juhudi zinazofanywa na walimu katika kuinua kiwango cha taaluma na kukabiliana na hali hiyo.

Akiwa katika Shule ya Msingi Nyachenda wakati wa ufuatiliaji huo, Afisa Elimu Taaluma, Loyce Malima, ameshuhudia matumizi ya mbinu anuai kutoka kwa walimu wa shule hiyo katika kukabiliana na uwepo wa wanafunzi wanaofanya mitihani wakiwa hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu.

Pamoja na jitihada hizo, mafanikio ya kielimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu yamekuwa yakichagizwa na miradi mbalimbali inayotekelezwa na mashirika ya Kimataifa yaliyojielekeza katika kuinua kiwango cha elimu.

Miongoni mwa mashirika hayo ni IRC linalotekeleza mradi wa Play Matter wenye maudhui ya kufundisha kwa kutumia michezo mradi ambao upo kwenye shule za Nyamganza, Mvugwe, Kumkambati, Kumtundu na Mkuyuni.

Aidha, kupitia maudhui hayo,Shirika la Save the Children linatekeleza mradi wa Play on kwenye shule za Kigadye, Heru Ushingo, Nyarugusu, Muungano, Jakaya Kikwete, Makere, Nyamidaho, Imanga na Kumlama.

Sambamba na mradi wa Play matter unaotekelezwa na IRC, shirika hilo linalohusika na uokoaji limekuwa "kinara" wa ufadhili katika kuboresha elimu kwenye halmashauri ya wilaya ya Kasulu kutokana na kuwepo kwa mradi wake mwingine wa Pop up. 

Mradi wa Pop up unaotumia teknolojia ya vishikwambi kufundishia na kujifunzia, upo kwenye shule nne za msingi ambazo ni Makere, Muungano, Nyarugusu na Nyachenda.
Pichani ni Afisa Elimu Taaluma, Bi.Loyce Malima akikagua ufundishaji na ujifunzaji katika darasa la Pop up lililopo kwenye shule ya Msingi Nyachenda akiwa na mwalimu mkuu wa shule hiyo, Malegesi Musiba.

Pamoja na mradi huo kulenga ufundishaji wa kusoma, kuandika na kuhesabu kwa kutumia teknolojia hiyo, mradi huo pia umekuwa kivutio kwa watoto na hivyo kupunguza tatizo utoro na la mdondoko.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news