KWARESMA TUJIKABIDHI KWA MUNGU

NA ADELADIUS MAKWEGA 

WAKRISTO wameambiwa kuwa Kipindi cha Kwaresma ni cha kusali zaidi, kipindi cha kuombeana mbele za Mungu na kipindi cha kujikabidhi kwa Mwenyezi Mungu. 

Hayo yamesemwa na Padri Paul Mapalala Parokiani Chamwino Ikulu katika Kanisa la Bikira Maria Imakulata, Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma katika misa Jumapili ya Pili ya Kwaresma Machi 5, 2023. 
“Kristo amekuja duniani kutukomboa na kutuokoa, inategenea kila mmoja uwazi wake na utayari wake wa kuwa na Kristo pamoja, atakapo kubali kuwa na Kristo katika kipindi chote cha Kwaresma na kwa kufanya hivyo ni kuzidi kumuelewa Mwenyezi Mungu, yeye nani, nani ni mwokozi na mkombozi wetu na nani ni mwenzetu? Kwaresma ni kipindi cha kutambua kuwa kila mmoja anayo mahitaji yake mbele ya Mungu, hakuna aliyekamilika.” 

Misa hiyo pia iliambatana na maombi kadhaa na mojawapo lilikuwa hili. “Uwashirikishe marehemu wetu utukufu wako.” 

Wakati wa matangazo ndani ya misa hiyo ilisomwa sehemu ya waraka wa Baraza la Maaskofu Katoliki yenye ujumbe wa Kwaresma wa mwaka 2023.
Kwa ujumla hali ya hewa ya eneo la Chamwino Ikulu kwa juma zima, mvua imenyesha mara mbili ambapo kidogo imesaida udongo kuwa mbichi na kama ikiendelea inaweza kuyasaidia mahindi ambayo hayajatoa mbelewele, hilo linaaminiwa na wakulima wengi wa eneo hili.
“Mahindi yaliyokwisha toa mbelewele hayawezi kuweka chochote hata kama yatakuwa hai, yatakuwa na mabunzi yenye punje chache sababu ikiwa kukosekana mvua kwa wakati.”

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news