NA AHMED MBILINYI
UJENZI wa Mahakama ya Mwanzo Nyakibimbili wilayani Bukoba, Mkoa wa Kagera umekamilika na tayari Mkandarasi kutoka Kampuni ya RK Solutions LTD, Mhadisi Gabriel Kami ameshakabidhi jengo jipya la Mahakama hiyo.

Viongozi kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Bukoba pamoja na viongozi wa eneo husika walikuwepo kushuhudia ukaguzi na makabidhiano hayo.

Kukamilika kwa ujenzi huo ni utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Mahakama 2020/2021 – 2024/2025 katika uboreshaji wa huduma zake kwa wananchi, ikiwemo kuimarisha miundombimu ya majengo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa makabidhiano hayo, Mhadisi Kami na Mhadisi Salehe wamesema jengo hilo limekamilika kwa asilimia 100, hivyo kushauri viongozi wa Mahakama kuanza kulitumia.
Picha ya pamoja kati ya Mkandarasi kutoka Kampuni ya RK Solutions, timu ya washauri elekezi wa mradi kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), timu ya Wahandisi kutoka Kitengo cha Ujenzi Makao Makuu ya Mahakama, viongozi kutoka Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba pamoja na viongozi wa eneo husika.
Akipokea jengo hilo kwa niaba ya Mtendaji wa Mahakama Kanda Bukoba, Bw. Lothan Simkoko, Kaimu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba, Mhe. Andrew Kabuka amewashukuru wataalamu hao kwa kukamilisha ujenzi huo. Ameahidi Mahakama itaanza kulitumia jengo hilo hivi karibuni.