NA MWANDISHI WETU
MAMA Janeth Magufuli, mke wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli ametunukiwa Tuzo ya Heshima nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kwa mchango wake alioutoa kwa mwenza wake alipokuwa madarakani.
Tuzo za M. T. KASALU zinatolewa na Taasisi ya LIZADEEL kwa kushirikiana na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Urithi ya DRC, UNESCO, UN-WOMEN na Asasi za Kiraia. Mama Janeth Magufuli ni miongoni mwa Washindi sita wa Toleo la Tatu la Tuzo hizo zilizokuwa zinawaniwa na wanawake 150.
Washindi wengine ni kutoka nchi za DRC (2), Senegal, Ufaransa na Marekani.
Anastahili pongezi Mamaetu, tutamkumbuka sana Hayati JPM
ReplyDelete