Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imewezesha miradi ya gridi ndogo ambazo zinazalisha umeme kwa kutumia nishati ya jua.
Miradi hii itaunga jumla ya wateja 11,720 na vijiji 46 vikiwemo visiwa 24 katika Ziwa Victoria. Kwa mujibu wa REA, miradi hii itaongeza upatikanaji wa umeme visiwani ambako kumekuwa hakufikiwi na umeme wa gridi kwa urahisi.