Ndani ya miaka miwili ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imekamilisha Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Kwanza ambao ulikuwa unatekelezwa mikoa yote ya Tanzania Bara.