NA DIRAMAKINI
LEO Machi 19, 2023 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan anaadhimisha miaka miwili ya uongozi wake madarakani tangu aapishwe rasmi Machi 19, 2021 akichukua nafasi ya Rais wa Awamu ya Tano,Dkt.John Pombe Joseph Magufuli ambaye alifariki Machi 17, 2021 wakati akiendelea na matibabu jijini Dar es Salaam.
Chini ya Rais Dkt.Samia, Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo kuleta suluhu ya changamoto kadha wa kadha kuanzia upande wa Diplomasia hadi kwenye kuimarisha demokrasia nchini. Chini ni sehemu ya salamu za pongezi kutoka kwa wadau mbalimbali nchini;
"Katika kipindi cha miaka miwili ya uongozi wake. REA imeendelea kutekeleza Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili katika mikoa 24, Ujazilizi wa 2A katika mikoa 9 pamoja na Mradi wa Vijiji Miji katika mikoa mitatu."