OR-TAMISEMI yatoa fursa kwa wahitimu Kidato cha Nne kufanya mabadiliko ya tahasusi (combination) na kozi za vyuo vya kati

OFISI ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) inatoa fursa kwa wahitimu wa elimu ya Sekondari Kidato cha Nne kufanya mabadiliko ya Tahasusi (COMBINATION) na Kozi za vyuo vya kati walizochagua kupitia fomu za Selform mwaka 2022.
Mabadiliko Yanafanyika kwenye Mfumo wa Uchaguzi wa Wanafunzi (Student Selection MIS) kupitia kiunganishi cha selform.tamisemi.go.tz

Tumia Namba yako ya Mtihani, Jina la Mwisho, Mwaka wa Kuzaliwa na Alama ya Ufaulu katika somo au swali utakaloulizwa.

Zoezi hili limeanza kufanyika kuanzia Machi 15, 2023 na mwisho ni Aprili 6,2023. Kwa changamoto yoyote, wasiliana nasi kwa barua pepe helpdesk@tamisemi.go.tz au piga simu 0262 160 210 na 0735 160 210.

Ili kujenga uelewa wa pamoja mzazi/mlezi unashauriwa kushirikiana na mtoto wako katika mabadiliko ya machaguo ya Tahasusi na kozi za vyuo vya kati.

Tangazo hili limeletwa kwenu na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news