Rais Dkt.Mwinyi afanya uteuzi ZRA

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amemteua Dkt.Hamed Rashid Hikmany kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA).

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Machi Mosi, 2023 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mhandisi Zena A.Said.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Dkt.Hikmany ni mstaafu katika utumishi wa umma na uteuzi wake umeanza Machi Mosi, 2023.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news