Rais Dkt.Mwinyi atoa mkono wa pole kwa familia ya marehemu Shaaban Iddi Mabrouk

MACHI 27, 2023 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi ametoa mkono wa pole kwa familia ya Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Bi. Dogo Iddi Mabrouk kufuatia kifo cha kaka yao huko Kwahani jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi (wa pili kulia) akiitikia dua iliyoombwa na Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Khalid Ali Mfaume (kulia) mara alipofika kutoa pole kwa familia ya marehemu, Bw.Shaaban Iddi Mabrouk,ndugu wa Makamu Mwenyekiti Jumuiya ya Wazazi, Bi.Dogo Iddi Mabrouk Kwahani Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi (kulia) alipofika kuwapa pole familia ya Makamu Mwenyekiti Jumuiya ya Wazazi, Bi.Dogo Iddi Mabrouk aliyefiwa na kaka yake marehemu, Bw.Shaaban Iddi Mabrouk, Kwahani Wilaya ya Mjini Mkoa Mjini Magharibi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akisalimiana na wananchi na wanafamilia ya marehemu, Bw.Shaaban Iddi Mabrouk, ndugu wa Makamu Mwenyekiti Jumuiya ya Wazazi, Bi.Dogo Iddi Mabrouk Kwahani Wilaya ya Mjini alipofika kutoa mkono wa pole.(Picha na Ikulu).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news