Serikali kuja na Jenga Kesho Nzuri

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imeamua kukuza sekta ya kilimo na kuifanya sekta hiyo kuingiza asilimia 10 ya ukuaji wa uchimi nchini ifikapo mwaka 2030.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya picha kutoka kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Mary Chatanda kabla ya kuhutubia Kilele cha Miaka miwili ya Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita.

Mheshimiwa Rais Dkt.Samia ameyasema hayo Machi 19, 2023 katika maadhimisho ya miaka miwili ya uongozi wake katika Uwanja wa Uhuru uliopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

 
Amesema, wameamua kuja mpango wa unaosema ‘Jenga Kesho Nzuri’ kwa ajili ya vijana kupitia kilimo wenye nia ya kujenga maisha mazuri kwa vijana.

Rais Dkt.Samia amesema, wakulima wengi kwa sasa ni vijana wa kiume, hivyo kesho watazindua shamba la kwanza la vijana Dodoma.

Pia amesema, kwa umoja wao watafanya kilimo cha kisasa, chenye tija na biashara pia na kwamba mashamba ya aina hiyo yataanzishwa nchi nzima.

Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amesema serikali itaendelea kununua vifaa vya matibabu ili huduma nyingi za kitabibu au matabibu bingwa zitolewe nchini.

Amesema, serikali imeshajenga hospitali, vituo vya afya na zahanati za kutosha na kazi iliyobaki ni kutengeneza watumishi watakaotoa huduma kwa wananchi. Rais Dkt.Samia amezungumzia mpango wa M-mama kuwa una nia kunusuru maisha ya mama wakati wa kujifungua nchini.

Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amesema,mpango huo umepata sifa duniani kote na sasa mashirika mbalimbali ya kimataifa wanakwenda kutekeleza mradi huo katika nchi mbalimbali huku Tanzania ikiwa tayari imeshaanza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news