Serikali yatoa maelekezo kwa TPSC na Taasisi ya UONGOZI

NA JAMES MWANAMYOTO

NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amekitaka Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) na Taasisi ya UONGOZI kuandaa programu za mafunzo zitakazowajengea uwezo kiutendaji watumishi wa umma na viongozi ili watoe huduma bora kwa wananchi na mchango katika maendeleo ya taifa. 
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akiwasili katika Chuo cha Utumishi wa Umma Kampasi ya Dar es Salaam kwa ziara ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma chuo hicho. 

Mhe. Kikwete ametoa maelekezo hayo jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara yake ya kikazi katika Chuo cha Utumishi wa Umma na Taasisi ya UONGOZI iliyolenga kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa taasisi hizo. 

Mhe. Kikwete amesema, watumishi wa umma na viongozi walio katika taasisi zote za umma wanahitaji kupata mafunzo yenye tija kwa ajili ya kukuza taaluma zao na kuongeza ufanisi kiutendaji, hivyo ni jukumu la Chuo cha Utumishi wa Umma na Taasisi ya UONGOZI kuhakikisha watumishi na viongozi wanapata mafunzo yatakayowawezesha kutekeleza majukumu yao kikamilifu. 
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akisalimiana na Menejimenti ya Chuo cha Utumishi wa Umma mara baada ya kuwasili chuoni hapo jijini Dar es Salaam kwa ziara ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma chuo hicho.

Mhe. Kikwete amesisitiza kuwa, Chuo cha Utumishi wa Umma kinatoa mafunzo kwa watumishi ambao wameshaajiriwa na Serikali, hivyo wanahitaji kuandaliwa programu nzuri za mafunzo zitakazoimarisha utendaji kazi wao. 

Sanjari na hilo, Mhe. Kikwete amekipongeza Chuo cha Utumishi wa Umma kwa kutoa mafunzo kwa watumishi wa umma wanaokaribia kustaafu ili kuwaandaa wawe na maisha mazuri baada ya kustaafu kuutumikia umma. 
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akiwa katika kikao kazi na Menejimenti ya Taasisi ya UONGOZI jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji wa watumishi wa taasisi hiyo.

“Binafsi naamini Chuo cha Utumishi wa Umma mnafanya jambo zuri kuwapatia mafunzo watumishi wanaokaribia kustaafu kwa mujibu wa sheria, hivyo mkijipanga vizuri nina uhakika hawataharibikiwa pindi wakistaafu,” Mhe. Kikwete amesisitiza. 
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akiwa katika kikao kazi na Menejimenti ya Taasisi ya UONGOZI jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji wa watumishi wa taasisi hiyo. 

Akizungumza na Menejimenti ya Taasisi ya UONGOZI, Mhe. Kikwete ameusisitiza uongozi wa taasisi hiyo kubuni programu za mafunzo ambazo zitawaandaa viongozi wa baadae, kama ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekusudia.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI, Bw. Kadari Singo akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi yake kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji wa watumishi wa taasisi hiyo kwa watumishi wa Taasisi ya UONGOZI jijini Dar es Salaam.

Mhe. Kikwete ameongeza kuwa, Rais wa Awamu ya Sita, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anatamani kuona Taasisi ya UONGOZI inatoa mchango wa kuwaandaa viongozi watakaoendeleza kazi nzuri iliyofanywa na uongozi wake. 

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amehitimisha siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi jijini Dar es Salaam ya kuzitembelea taasisi zilizo chini ya ofisi yake ili kuhimiza uwajibikaji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news