NA ANGELA MSIMBIRA
SERIKALI imetoa siku 21 kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha nne mwaka jana kubadili tahasusi na kozi za vyuo vya kati ili kufanya chaguzi sahihi.
Hayo yamesemwa na Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Dkt.Charles Msonde jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu fursa ya kubadili Tahasusi kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha nne mwaka 2022.
Amesema kuwa, Serikali imetoa fursa hiyo kutokana na baadhi ya wanafunzi walifanya chaguzi awali kuwa na mitazamo tofauti ambayo inahitaji kufanya marekebisho baada ya matokeo kutoka Januari 19, mwaka huu.
“Wajibu wa TAMISEMI ni kuwapangia shule au vyuo mbalimbali ili kuanza masomo Julai mwaka huu, kwa kutumia mfumo wa kompyuta, ili hili lifanyike lazima wawe wamefanya machaguo yao wanayotaka kusoma, vyuo au shule na fani gani wanazipenda,”amesema Dkt. Msonde.
Amesema, Serikali imewapa fursa wanafunzi hawa kufanya marekebisho ya tahasusi zao kama inafaa, lengo ni kufanya chaguzi sahihi kadiri walivyofaulu, baada ya hapo tutaamua kupitia chaguzi walizofanya, lakini kwaa wale waliochagua sahihi awali na kuona ni sahihi tangazo hili haliwahusu.
“Tunatoa fursa inawezekana baada ya matokeo ameona mtazamo mwingine anahitaji kufanya marekebisho, au anataka kusoma kitu kingine badala ya alichochagu, hivyo tunatoa siku 21 kuanzia leo (Machi 14, 2023) maana mfumo utakuwa wazi zoezi litaisha Aprili 6 tunaamini kipindi hichi kinatosha kufanya marekebisho,”amesema.
Dkt Msonde ametoa rai kwa wanafunzi kufanya marekebisho kama ni lazima kufanya hivyo maana hakutakuwa na mabadiliko mengine baada ya wiki tatu(siku 21)kuisha.
Aidha, amewataka kufanya uchaguzi kwa kuzingatia ufaulu wa masomo kwa sababu utakuwa wa ushindani kwenye tahasusi zilizochaguliwa.
“Hakikisha unachagua masomo unayoweza ili usichague nyingine ukashindwa ukakosa,”alisisitiza.