Tunawekeza katika miundombinu bora kila kaunti nchini-Rais Ruto

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Kenya, Mheshimiwa Dkt.William Ruto, Ijumaa iliyopita alizindua ujenzi wa barabara ya Gamba-Kegogi huko Kaunti ya Kisii.

Barabara hiyo ya kilomita saba itaunganisha Kisii hadi Ahero huko Oyugis na kurahisisha usafirishaji wa watu, bidhaa na huduma sokoni.
Mheshimiwa Rais Dkt.Ruto pia alizindua mradi wa ufikivu wa njia ya Sirari na uboreshaji wa usalama barabarani na ujenzi wa sehemu ya pili ya barabara ya Kisii Ahero A1. Mkuu wa Nchi alisema, Serikali haitavumilia wakandarasi wanaofanya kazi kwa uvivu, kwani inahitaji kazi ifanyike kwa wakati ili wananchi waweze kutumia miundombinu hiyo kujiletea maendeleo.

“Nimefanya mazungumzo na viongozi wenu na tumekubaliana kwamba tutashirikiana kukamilisha miradi yote iliyokwama ili tubadilishe sura ya Kisii na kaunti kwa ujumla,"alisema.
Mheshimiwa Rais Dkt.Ruto alisema, Serikali inawekeza pakubwa katika uchumi wa kidijitali, usindikaji wa mazao ya kilimo na uongezaji thamani na makazi ili kuzalisha ajira.

Pia Mheshimiwa Rais Dkt.Ruto alisema, serikali ya kitaifa na serikali ya kaunti ya Kisii zitashirikiana kuunda Hifadhi ya Viwanda ili kukuza biashara ya kilimo katika kaunti hiyo.

"Hifadhi itatusaidia katika kuongeza thamani, kujumlisha na kuweka alama salama kwa wakulima," alisema.

Waliohudhuria katika hafla hiyo ni Makamu wa Rais Rigathi Gachagua,Waziri wa Ujenzi, Kipchumba Murkomen, mwenzake wa Elimu, Ezekiel Machogu, magavana Simba Arati (Kisii) na Amos Nyaribo (Nyamira), wabunge,makatibu wakuu ni miongoni mwa viongozi wengine.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news