Wafugaji wa jongoo bahari kuneemeka

NA MWANDISHI WETU

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Mheshimiwa David Silinde amefunga mafunzo ya ufugaji jongoo bahari yaliyokuwa yakifanyika kwenye Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Kampasi ya Lindi na kuratibiwa na wizara hiyo chini ya Wakala ya Mafunzo ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) kampasi ya Mkindani mkoani Mtwara.

Mafunzo hayo ambayo yamehusisha washiriki 68 yamefanyika kwa muda wa siku 10 ambapo kwenye hotuba yake ya kufunga mafunzo hayo, Mheshimiwa Silinde amewataka kutumia ujuzi walioupata kuzalisha jongoo bahari wa kutosha ili kuongeza kipato chao na Taifa kwa ujumla.

“Mafunzo haya ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia (Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan) aliyoyatoa kwenye kilele cha Maonesho ya Nanenane, mwaka jana Mbeya ambapo alielekeza sekta zote za uzalishaji ikiwemo Sekta ya Uvuvi kushirikisha Wadau mbalimbali ikiwemo sekta binafsi kuwawezesha wananchi waweze kujiajiri,”amesema.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga mbali na kuishukuru Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kutekeleza ahadi yake ya kuwezesha mafunzo hayo, amewataka wananchi wote mkoani humo kujiingiza kwa wingi kwenye uzalishaji wa mazao ya uvuvi ikiwemo jongoo bahari ili kuendelea kuupandisha uchumi wa mkoa kwa ujumla.

“Kilo moja ya jongoo bahari inauzwa zaidi ya shilingi 180,000, sasa kama wananchi wote tutajikita kwenye shughuli hii bila shaka tutafika mbali sana na ninawaomba wenyeviti wa halmashauri, mstahiki meya na wakurugenzi mliopo hapa.

"Ile asilimia 10 ya Wanawake na Vijana ni bora wapewe wahitimi hawa wa mafunzo kwa sababu wanafanya shughuli ambayo inajulikana na faida yake inaonekana wazi,”amesema DC huyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news