Wafurahia elimu ya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji dhidi ya watoto kutoka Polisi

NA MWANDISHI WETU

WANAFUNZI wa Shule ya Sekondari Wiza wilayani Mbozi wamelishukuru Jeshi la Polisi kupitia Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Songwe baada ya Mtendaji wa Dawati hilo Mkaguzi wa Polisi Debora Mhekwa kufika shuleni hapo na kuwapa elimu juu ya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji dhidi ya watoto.

Kupitia elimu hiyo wanafunzi hao walipata fursa ya kuuliza maswali kama ifuatavyo; 1.Huduma za dawati la jinsia zinatolewa kwa bei gani? Walijibiwa kuwa huduma hiyo hutolewa bure kwa ni haki ya mwananchi kisheria.
2. Na, Je? Kama umetendewa ukatili wa kijinsia na msimamizi wa sheria (mfano askari) utapataje msaada wa kusheria? Swali hili nalo walijibiwa kuwa hakuna aliye juu ya sheria, hivyo wasisite kutoa taarifa endapo itatokea kutendewa hivyo bila kujali wadhifa wa mtu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news