WANANCHI MUSOMA VIJIJINI WAKISHIRIKIANA NA PROF.MUHONGO WAAMUA KUJENGA MAABARA TATU NDANI YA MIEZI MITATU

NA DIRAMAKINI

MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini, mkoani Mara, Prof. Sospeter Muhongo ameshirikiana na wananchi wa Kata ya Bukumi katika harambee yenye lengo la kupata fedha za ujenzi wa maabara tatu za Masomo ya sayansi (Fizikia, Kemia na Baiolojia za Mtiro Sekondari ambapo Prof. Muhongo ameanza kwa kuchangia mifuko 150 ya saruji. 
Hayo yamebainishwa kupitia taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini leo Machi 11, 2023. Huku ikieleza kuwa harambee hiyo ilifanyika shuleni hapo Mtiro Sekondari Machi 9, 2023 Ambapo Wanavijiji wa Kata ya Bukumi wameamua kujenga Maabara 3 za Masomo ya Sayansi kwenye Sekondari yao ya Kata, Mtiro Sekondari.
Kata ya Bukumi ina vijiji vinne ambavyo ni Buira, Bukumi, Buraga na Busekera huku takwimu za Mtiro Sekondari ilifunguliwa Mwaka 2006, ikiwa na idadi ya wanafunzi 682, idadi ya walimu ni 17 (13 wenye ajira ya Serikali na 4 wa kujitolea)hakuna Maktaba na pia hakuna Maabara hata moja ya Masomo ya Sayansi.

Taarifa hiyo imesema,"wanafunzi 17 kati ya 110 wa Kidato cha Tatu (Form III), 15.5%, ndio wanasoma Masomo ya Sayansi. wanafunzi 25 kati ya 123 wa Kidato cha Nne (Form IV), 20.3%, ndio wanasoma Masomo ya Sayansi. wanafunzi 5 kati ya 682, ndio wamechangia chakula cha mchana,"imeeleza.
"Prof. Muhongo alianza kwa kutoa saruji mifuko 150. Huku michango ya Wanavijiji iliongozwa na Diwani wao, Mhe Munubhi Musa, Wazaliwa wa Kata ya Bukumi nao wameanza kuchangia. Fedha Taslimu shingi 494,000.Fedha ahadi) Shingi Mil. 4,493,000, Saruji Mifuko 26, Mchanga Lori 5."

"Michango ya Mbunge wa Jimbo, ameanza kwa kutoa Saruji Mifuko 150, ujenzi kuanza jumatatu 13.3.2023 Wanavijiji na Viongozi wao wa Kata ya Bukumi wameamua kuanza kutekeleza mradi huu mara moja. na mchanga wa kuanzia kazi tayari umesombwa. Saruji Mifuko 75 kati ya 150 iliyotolewa na Mbunge wa Jimbo tayari imefikishwa shuleni,"imesema taarifa hiyo.
"Ifikapo Juni 2023, maabara 3 ziwe zimekamilika. Mawasiliano ya kutoa mchango wako Headmaster. Mtiro Sekondari simu 0758 487 478," imesema taarifa hiyo. 

"Wanavijiji wa Kata ya Bukumi wanaomba sana Wadau wa Maendeleo wajitokeze kuchangia utekelezaji wa mradi huu ambao ni muhimu sana kwa uboreshaji wa miundombinu ya elimu itolewayo Mtiro Sekondari - tunatanguliza shukrani zetu za dhati kwa wachangiaji wote."
"Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini anaendelea na kampeni yake ya kuhamasisha na kuchangia ujenzi wa Maabara 3 za Masomo ya Sayansi kwenye Sekondari zote za Jimboni mwao."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news