WATUMISHI WANAWAKE BRELA WAPATIWA MAFUNZO YA UONGOZI

NA MWANDISHI WETU

WATUMISHI wanawake viongozi wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), wametakiwa kuzingatia mambo ya msingi katika utendaji kazi ili kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Rai hiyo imetolewa tarehe 9 Machi, 2023 na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya BRELA, Prof. Neema Mori, wakati wa mafunzo maalum ya uongozi kwa watumishi wanawake viongozi wa Taasisi hiyo katika hoteli ya Hyatt, jijini Dar es Salaam. 

Prof. Mori ameyataja mambo ya msingi anayopaswa kuyazingatia kiongozi ni pamoja na nidhamu, utii, bidii, kujituma, pamoja na mawasiliano mazuri na wengine.
"Kama viongozi mkiyazingatia haya mtafanya maamuzi sahihi yenye kuleta tija,"ameleeza Prof. Mori.

Prof. Mori ameeleza pia kuwa viongozi wanawake wanapaswa kujitambua na kuziishi ndoto zao kwa kutekeleza majukumu yao na kufikia malengo waliyojiwekea.
“Kila mwanamke ni kiongozi katika nyanja tofauti, hivyo ni vyema kufahamu nafasi yako mahali ulipo, hii itasaidia kujiongoza na kuwaongoza wengine,”amesisitiza Prof. Mori.

Amesema, mafunzo hayo maalum yamelenga katika kupeana elimu na kujadiliana juu ya masuala muhimu ya kuzingatia kama viongozi na namna mwanamke anaweza kuwa kiongozi hodari na mwenye kufanya majukumu yake pasipo kuwa na uoga wowote.
Prof. Mori amefafanua kuwa,suala la nidhamu, kuishi kwa usawa na kufanya matendo yenye kuongeza tija katika jamii kama viongozi yatawafanya wakumbukwe na wengine kufuata nyayo zao.

Ameongeza kuwa ni vema kutambua aina ya watu wanaowaongoza kwani kuna watu wa wenye tabia zinazotofautia ambazo wakati mwingine huleta ugumu katika uongozi hivyo, mnapaswa kujua ni jinsi gani mnaweza kusaidiana. 
Mafunzo haya ya siku moja yameandaliwa na Prof. Mori kwa kushirikiana na uongozi wa Taasisi katika kuwajengea uwezo wanawake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news