NA MWANDISHI WETU
WAZIRI wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) amekitaka Kiwanda cha kutengeneza viuadudu (TBPL) kuhakikisha kinajitangaza ndani na nje ya nchi ili kuongeza wigo wa masoko kwa kuuza bidhaa hiyo ya kipekee ambayo inazalishwa hapa nchini.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji pamoja na wajumbe wengine wakipewa maelezo na Jovin Magayane (mwenye koti jeupe), Mtaalam wa Maabara wa Tanzania Biotech Products Limited (TBPL) namna sampuli mbalimbali zinavyopimwa ndani ya maabara ya kiwanda hicho ili kuzalisha viuadudu vya kuangamiza mazalia ya mbu.
Dkt.Kijaji ameyasema hayo leo Machi 29, 2023 alipotembelea kiwanda hicho kilichoko Kibaha Mkoani Pwani kushuhudia namna uzalishaji wa dawa za viuadudu unavyofanyika kiwandani hapo.
Akiwa kiwandani hapo Dkt. Kijaji amekiagiza kiwanda hicho kuhakikisha kinajitangaza kwa nguvu zote ili kupata masoko ya ndani na nje ya nchi badala ya kutegemea soko la ndani ambalo kwa kiwango kikubwa limeonekana kuwa ni la kusuasua.

Aidha, Waziri Kijaji ameiagiza TBPL kushirikiana na TANTRADE katika kuhakikisha dawa hizo zinatangazwa katika masoko ya ndani na nje ya nchi pamoja na kuwa na mipango mikakati ya masoko itakayofanikisha utoaji wa elimu juu ya matumizi ya dawa hizo na faida zake kufika kwa watanzania wengi.

Katika hatua nyingine Mapunda pia alibainisha juu ya nia ya kiwanda hicho kuanza rasmi uzalishaji wa viuatilifu vya mazao ili kupambana na wadudu waharibifu wa mazao ambapo dawa hizo mara baada ya kufanyiwa majaribio zimeonyesha mafanikio makubwa katika kupambana na wadudu hao ambao ni hatari kwa ustawi wa sekta ya kilimo hapa nchini.

