NA JOHN MAPEPELE
SERIKALI imewataka wananchi wote nchini kutumia boti ya kisasa ya Utalii iliyozinduliwa rasmi Machi 14, 2023 ili kukuza utalii wa ndani.
Kauli hiyo ameitoa Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mohamed Mchengerwa Kilwa Masoko kwenye hafla ya uzinduzi wa boti maalum ya Utalii ijulikanayo kama TAWA SEA CRUISER inayomilikiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA).


Katika hatua nyingine Mhe. Waziri ametembelea maeneo ya kitalii ya mji mkongwe wa kihistoria wa Kilwa na kujionea vivutio vya utalii vya asili kama msikiti wa Karne ya 12 magofu ya kale na jumba la mfalme.

Pia Kisiwani hapo Mhe Mchengerwa ameshuhudia boti ya kisasa ya Le Jacques Cartier Ponant kutoka nchini Ufaransa ikitia nanga katika fukwe ya Kilwa Kisiwani na baada ya muda mfupi kuanza kuwashusha wageni.