NA MWANDISHI WETU
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akiongozana na Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu wametembelea mabanda ya taasisi pamoja na wadau yakiongozwa na banda la Wizara ya Afya kwa lengo la kujua huduma zinazotolewa katika taasisi hizo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kifua Kikuu Duniani tarehe 24 Machi, 2023.

Maadhimisho hayo ya Kifua Kikuu hufanyika kila Mwaka tarehe 24 ambapo mwaka huu yamefanyika Kitaifa katika Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu yenye kauli mbiu isemayo “Kwa Pamoja Tumaweza Kutokomeza Kifua Kikuu Nchini Tanzania”.