Waziri Simbachawene:Tutumie rasilimali zilizotolewa kufanya kazi

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. George Simbachawene, amewataka watumishi wa ofisi hiyo kutumia rasilimali zilizotolewa kufanya kazi kwa bidii na ufanisi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. George Simbachawene (katikati), kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa ofisi yake Dkt. Jim Yonazi na kulia kwake ni Mwenyekiti wa TUGHE tawi la Ofisi hiyo, Bi. Numpe Mwambenja wakiwa katika picha ya pamoja ya watumishi wa Ofisi ya Waziri baada ya kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo kilichofanyika Machi 14, 2023 Jijini Dodoma. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU).

Mhe.Simbachawene ameyasema hayo leo Machi 14, 2023 jijini Dodoma wakati wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi la Ofisi hiyo kilichokutana kwa lengo la kujadili utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2022/23 pamoja na makisio ya matumizi ya fedha kwa mwaka wa fedha 2023/24.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. George Simbachawene akizungumza katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Waziri Mkuu (kulia) ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Dkt. Jim Yonazi kilichofanyika Machi 14, 2023 Jijini Dodoma.

Aliendelea kusema kuwa, Baraza la Wafanyakazi ni jukwaa muhimu sana mahala pa kazi kwani ni kiunganishi kati ya Menejimenti na Watumishi, na alibainisha kuwa, Serikali inazingatia sana suala la Wizara na Taasisi zake kuwa na mabaraza ya wafanyakazi kwani, yanaanzishwa kisheria kwa madhumuni ya kuishauri Serikali katika ngazi za Idara, Taasisi na Wizara ili kuweza kusimamia kazi na rasilimali watu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. George Simbachawene akizungumza katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Waziri Mkuu (kulia) ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Dkt. Jim Yonazi kilichofanyika Machi 14, 2023 jijini Dodoma.

Alibainisha kuwa mabaraza haya yana majukumu ya kulinda haki na wajibu wa waajiri na wafanyakazi, kutoa ushauri kuhusu kujenga hali bora za kazi, masilahi ya wafanyakazi na kusimamia haki na ustawi katika sehemu za kazi. 

Wajibu wa mabaraza haya kama vyombo vya ushauri na usimamizi ni kuhakikisha kuwa waajiri na watumishi wanatambua wajibu na haki zao, pia wanazingatia maadili ya utumishi wao ili kuleta matokeo ya utendaji wa kazi yenye tija, staha na upendo.
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) wakifuatilia kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo kilichofanyika Machi 14, 2023 jijini Dodoma.

Ameshauri menejimenti kupitia baraza hilo la wafanyakazi, kuwa na utaratibu mzuri wa kuwapongeza wafanyakaki wanaotekeleza majumu yao kwa uweledi, ”kuna watumishi ambao kufaya kazi kwa weledi na biidii, na kuwahudumia wananchi kwao ni kama sehemu ya ibada,”alifafanua

Aliendelea kusema kuwa Utumishi wa umma wa zama hizi ni watu wenye ueledi,wasomi na wenye wasifu mkubwa,lakini wanashindwa kuuonesha kutokana na mazingira kutokuwa rafiki,aliwaasa watumishi wa ofisi hiyo kufanya kazi ya umma kwa bidii.”Jukumu kubwa kwa ninyi viongozi ni kuwahudumia wadogo ili waweze kuleta matoke,”alisema Mhe. Simbachawene.
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) wakifuatilia kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo kilichofanyika Machi 14, 2023 jijini Dodoma. 

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Dkt. Jim Yonazi aliwashukuru watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kutekeleza majukumu yao na kusimamia shughuli mbali mbali za serikali kwa kujituma na kwa ufanisi mkubwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news