NA MWANDISHI WAF
WAZIRI wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu, Machi 25, 2023 amewasili mkoani Kagera kwa lengo la kujua hali inavyoendelea juu ya ugonjwa wa Marburg ulioibuka hivi karibuni mkoani humo.
Aidha, Waziri Ummy amepokea taarifa kwa timu inayoongozwa na Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Tumaini Nagu aliyoiagiza kuendelea kufuatilia ugonjwa huo mara baada ya kugundulika Mkoni Kagera.
Ikumbukwe kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya ilitoa taarifa juu ya uwepo wa ugonjwa wa MARBURG katika Wilaya ya Bukoka Vijijini mkoani Kagera ambapo watu watano wamefariki kutokana na ugonjwa huo.
Ikumbukwe kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya ilitoa taarifa juu ya uwepo wa ugonjwa wa MARBURG katika Wilaya ya Bukoka Vijijini mkoani Kagera ambapo watu watano wamefariki kutokana na ugonjwa huo.
Aidha,bado Serikali inatoa wito kwa Watanzania kuchukua tahadhari na kutoa taarifa endapo utapatwa na dalili kama za homa, kutapika, kutokwa damu maeneo mbalimbali ya mwili na figo kushindwa kufanya kazi.