Waziri wa Afya ateta na Balozi wa Marekani nchini

NA MWANDISHI WAF

WAZIRI wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu leo amekutana na Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dkt. Michael Battle kwenye ofisi za Wizara jijini Dodoma.
Katika mazungumzo yao Waziri Ummy amemwambia Balozi huyo kwamba Serikali ya Tanzania inawashukuru Marekani kwa kuendelea kushirikiana hususani kwenye maboresho katika sekta ya afya nchini.

Aidha, Waziri Ummy amesema Tanzania inafanya vizuri katika jitihada ya kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano.
Amesema, bado kuna changamoto ya ubora wa huduma na gharama za matibabu kwa wananchi hivyo Serikali inakuja na Bima ya Afya kwa Wote ili kuwaondolea adha ya matibabu wananchi wake.

Kwa upande wa watumishi Waziri Ummy amesema wana uhaba wa watoa huduma kwa asilimia hamsini na wanaendelea kuajiri watumishi kila mwaka.
Kwenye eneo la HIV amesema wanafanya vizuri katika eneo la 95-95-95 na Malaria na TB bado wanaendelea na mapambano dhidi ya magonjwa hayo.

Naye, Balozi wa Marekani,Dkt. Battle amesema kupitia CDC wataendelea kusaidia kuboresha afya za wananchi kupitia sekta ya afya na kutoa mafunzo kwa watoa huduma za afya ngazi ya jamii pamoja na wataalamu wa maabara katika uchunguzi wa magonjwa mbalimbali ikiwemo magonjwa ya milipuko.
Hata hivyo, Balozi huyo amempongeza Waziri Ummy kwa kusimamia vizuri Wizara ya Afya hususani katika mapambano ya magonjwa ya mlipuko.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news