Wizara ya Ardhi,Sinotec wasaini hati ya makubaliano kwa ajili ya Mradi wa Nyumba za Maendeleo Zanzibar

NA MWANDISHI WETU

WIZARA ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi (WAMM) jana imesaini Hati ya Makubaliano na kampuni ya Sinotec kwa ajili ya Mradi wa Nyumba za Maendeleo Zanzibar.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi (WAMM) Dkt. Mngereza Mzee Miraji (kushoto ) na Naibu Meneja Mkuu wa Kampuni ya SINOTEC Jin Hua (kulia) wakisaini hati ya Makubalino (MoU) ya Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Maendeleo Zanzibar, hafla hiyo imefanyika jana katika ukumbi wa WAMM Maisara, Unguja.

Hafla ya utiaji saini imefanyika jana katika ukumbi wa wizara hiyo ambapo kwa upande wa Wizara alisaini Katibu Mkuu Dkt Mngereza Mzee Miraji na kwa kampuni ya Sinotec alisaini Naibu Meneja Mkuu Jin Hua. 

Akizungumza mara baada ya utiaji wa saini hiyo Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Mngereza amesema makubaliano hayo ni hatua ya mwanzo katika utekelezaji wa mradi huo, ambapo lengo kuu ni kutekeleza Sera ya Makaazi bora kwa wananchi kupitia wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Zanzibar.
Naye Naibu Meneja Mkuu wa kampuni hiyo Jin Hua amesema amefarajika kupata fursa hiyo ya Kufanya kazi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Wizara ya Ardhi ili kuifanya jamii kuwa na Makaazi bora ya kuishi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba Zanzibar (ZHC),Mwanaisha Ali Said amesema ujio wa kampuni hiyo ni faraja kwa Serikali kwani ujenzi wa Mradi wa Nyumba za Maendeleo utaweza kuondoa uhaba wa nyuma Zanzibar.

Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Zanzibar inaendelea na hatua mbalimbali za utiaji saini ya miradi ya Ujenzi wa Nyumba za Maendeleo ambapo awali ilitiliana saini na kampuni ya ASER Construction and Technology Ltd.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news