NA DIRAMAKINI
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi ametembelea eneo la Shehia ya Kama Wilaya ya Magharibi A, Mkoa wa Mjini Magharibi kukagua ujenzi wa mradi wa mfereji mkubwa wa maji ambao ulikuwa kero ya muda mrefu.
Wananchi wa Shehia hiyo walimshukuru Rais Dkt.Mwinyi kwa kutekeleza ahadi na kutatua changamoto hiyo sugu ambayo imedumu kwa muda mrefu, mradi huo unatarajiwa kumalizika kabla ya msimu wa mvua.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akitoa maelekezo mACHI 4, 2023 kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ,Mhe. Masoud Ali Mohammed, wakati alipofanya ziara ya kushtukiza kutembelea.Mradi wa Ujenzi wa Soko la Kisasa Chuini Wilaya ya Magharibi “A”Unguja.(Picha na Ikulu).
Wakati huo huo Rais Dk. Mwinyi alitembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Masoko ya kisasa maeneo ya Chuini kwa Nyanya, Soko la Jumbi na Mwanakwerekwe.
Dk.Mwinyi amewaagiza wakandarasi wa Masoko hayo kukamilisha ujenzi ifikapo Mwezi Novemba ili kuyafungua Disemba, mwaka huu.