NA DIRAMAKINI
JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya limethibitisha kutokea kwa ajali iliyohusisha basi la Kampuni ya Abood lililokuwa likitokea jijini Mbeya kwenda Dar es Salaam.
Basi hilo limepata ajali maeneo ya Mswisi wilayani Mbarali ambapo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga amesema, “Ni kweli ajali imetokea na basi limelalia ubavu mmoja, kuna majeruhi kadhaa ambao wamepelekwa hospitali.
“Inavyoonekana chanzo cha ajali ni dereva kukosa umakini wakati akiwa katika mwendo kasi, bahati mbaya dereva amekimbia na hatujui alipo, abiria wengine wameondoka kwa usafiri mwingine.Tunaendelea kulifanyia uchunguzi basi kisha tutatoa taarifa kamili baadaye.”
Aidha, taarifa za awali zinadokeza kuwa,majeruhi watano katika ajali hiyo wamekimbizwa katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya (MZRH) kwa matibabu.
Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Kanali Denis Mwila amesema kuwa, ajali hiyo imetokea majira ya saa moja asubuhi katika barabara kuu ya Tanzania na Zambia (Tanzam).
Kanali Mwila amesema kuwa, taarifa za awali zinaeleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi hilo ambaye amekimbia baada ya ajali kutokea, kutaka kulipita gari lingine lililokuwa mbele yake na kusababisha ajali hiyo.
“Tunashukuru Mungu hakuna kifo hata kimoja zaidi ya watu watano kupata majeraha wakiwepo wanawake wawili na wanaume watatu ambao wamekimbizwa kupatiwa matibabu katika Hosptali ya Rufaa ya Kanda (MZRH),” amesema Kanali Mwila.